" Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo & Mitazamo ya wengine. Mchango wako katika kazi yoyote ulenge kujenga jamii yenye Kujitambua, Kujithamini na Kujiwajibisha "

 
Thursday, June 01, 2006

 wananchi waujadili Muungano

NILIPIGWA na butwaa niliposoma habari kuu ya gazeti la mwananchi la Jumatatu, kuhusu kauli ya Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha.

Nilipigwa na butwaa kwa sababu mtu mmoja ametoa kauli mbili tofauti katika kipindi kisichozidi siku 8.

Wiki iliyopita, Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Waziri Kiongozi Nahodha walikutana jijini Dar es Salaam kujadili kero za Muungano.

Baada ya kikao chao kilichoshirikisha mawaziri kutoka pande zote mbili za muungano, viongozi hao walikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza yale waliyokubaliana.

Imani yetu ilikuwa kwamba makubaliano yoyote watakayoyafikia, msingi wake ni maoni ya wananchi.

Lakini imeshangaza kwa upande wa Zanzibar, inaonyesha kama kwamba Waziri Kiongozi alikurupuka tu na kukubaliana na mengi ya yaliyojadiliwa bila kuzingatia maslahi ya Zanzibar na bila kutilia maanani matakwa ya Wazanzibari.

Wazanzibari wa kawaida wanasema mengi tu kuhusu Muungano, nilidhani maoni yao yangezingatiwa wakati wa majadiliano ya viongozi wa juu.

Ni kutokana na mambo kama haya ya kurukana na kuonekana kwamba upo upande umeemewa na umegubikwa na upande mwingine, ndio maana wananchi waliotoa maoni yao kuhusu Muungano walisema kwamba umefika wakati mjadala kuhusu Muungano usiwe wa Serikali pekee, uwekwe wazi, uratibiwe vizuri ili vyama vya siasa, asasi zisizo za kiserikali na vyama mbalimbali vya kijamii vishiriki kujadili suala hilo kwa sababu ni suala linaloihusu jamii nzima.

Kwa kufanya hivyo ingeonekana wazi kwamba kwa njia moja jamii imeshirikishwa katika kujadili mustakbali wa nchi yao.

Sio kama wananchi hawawaamini viongozi wao wa Serikali zote mbili katika kufikia maamuzi yanayogusa hisia za wananchi, lakini katika mfumo wa demokrasia ya uwakilishi, hakuna ubaya wowote kushirikishwa watu wengine katika kufikia maamuzi yaliyoazimiwa na Serikali.

Binafsi nadhani njia muafaka ya kuratibu maoni ya wananchi ni kuwaruhusu wananchi watoe maoni yao kupitia kura ya maoni.

Huwa najiuliza swali, hivi ni kwa sababu gani kila mara kunapokuwa na msukumo kutoka kwa wananchi wakiwataka viongozi wao waitishe kura ya maoni ili wananchi wapate kutoa maoni yao moja kwa moja bila kupitia kwa wawakilishi wao, Serikali huwa inapata kigugumizi, kwani ina wasiwasi gani?

Kutoa kura za maoni kuhusu masuala mbalimbali katika jamii ni haki ya wananchi na nadhani Serikali haitaumia chochote kama itaruhusu kutumika kwa utaratibu huo katika suala la Muungano.

Inatia wasiwasi kuona Serikali ikiogopa kusikiliza maoni ya wananchi wake, matokeo yake ndiyo kama haya ya Waziri Kiongozi Nahodha kujaribu kurudisha matamshi aliyoyatoa baada ya kupata shinikizo kubwa kutoka kwa Wazanzibari.

Baada ya majadiliano yale Wazanzibari walimuuliza Nahodha ana dhamira gani kwao? Kwani Wazanzibari hawawezi kumiliki mafuta yatakayozalishwa visiwani mwao?

Ikiwa madini si suala la muungano, kwanini mafuta ya kutoka Zanzibar yawe ni suala la Muungano?

Mwanzo alikubali kwamba mafuta ya Zanzibar yawe ya muungano na kwa pamoja waliamua shirika la Petroli nchini (TPDC) liwe la Muungano na wajumbe wake watoke pande zote mbili za Muungano.

Kwa miaka zaidi ya 40 shirika hilo lilikuwa la Serikali ya Muungano pekee, ghafla maamuzi yamepitishwa liwe la Muungano vyereje? Kwa sababu kumevumbuliwa dhahabu (mafuta) Zanzibar?

Hayo ndiyo Wazanzibari wa kawaida tu wanayojiuliza. Wanasema walidhani kwamba kwa kuwa madini na maliasili si suala la Muungano, petroli nayo isingeingizwa katika masuala ya Muungano.

Binafsi nadhani ni makosa kufikiri kwamba mawazo yoyote kinzani ni mawazo ya vyama vya upinzani na kwamba mwanachama wa chama tawala hapaswi kuhoji lile analoona kuwa si sawa, kwa kuwa viongozi wake wameona kwamba hilo ndilo la sawa.

Nadhani ifike wakati masuala ya Kitaifa yasipewe sura ya upinzani, waachiwe watu wawe huru kutoa mawazo yao, sidhani kama yupo Mtanzania mwenye akili timamu asiyetumiwa na mafisadi wasioitakia mema nchi hii, atatoa mawazo kwa shabaha ya kuvuruga.

Waachiwe watu watoe mawazo yao kuhusu mfumo wa muungao au makubaliano ya Muungano, bila kupigwa muhuri kwamba ni wapinzani, kwani nina wasiwasi itakuwa vigumu kupata mawazo ya kujenga (constructive ideas) ikiwa watoa mawazo watajengewa dhana ya kwamba mawazo ya watu Fulani, hayastahili kuchukuliwa kama mawazo ya kujenga, hata kama mawazo hayo yatakuwa mazuri kwa kiasi gani ama yatakuwa yana maslahi kwa Taifa kwa kiasi gani.

Suala la mafuta ni miongoni mwa masuala mengi tu ya kiuchumi ambayo Wazanzibari wanahisi kwamba wamenyang’anywa, basi kabla ya kuyatolea maamuzi masuala kama hayo, kwanini basi kwamba viongozi na wataalam wetu wasiende kujifunza katika mataifa yaliyoungana na kufanikiwa.

Wenyewe walisema wanakusudia kwenda kujifunza katika nchi za Scotland, Norway na Canada, sasa imekuwaje wakaanza kutoa maamuzi hata kabla ya kupata hayo mafunzo waliyodhamiria kuyapata?

Nilidhani kikao kile cha mawaziri kilikuwa ni kikao cha kwanza tu cha kuangalia joto ya jiwe, sikufikiria hata kidogo kama kitakuwa ni kikao cha kutoa maamuzi, ingawa kisheria wanayo mamlaka hiyo ya kutoa maamuzi kwa niaba ya wananchi wa nchi hizi mbili zilizoungana.

Masuala haya yanapaswa yaangaliwe kwa kina kwani kikao cha siku moja cha Mawaziri hakiwezi kutoa majibu ya maswali magumu waliyonayo wananchi, mojawapo likiwa ni yepi yaendelee kuwa mambo ya Muungano na yepi yasiwe mambo ya Muungano.

KUHUSU MIMI

JINA:Hawra Shamte
MAKAZI:Dar es salaam
NCHI:Tanzania
KAZI:Mwandishi

KUELEKEA BUNGE LA BAJETI 2006

QuickTopic free message boards
Bonyeza hapa ili uweze kuelezea: NINI MTAZAMO WAKO JUU YA BAJETI IJAYO YA MWAKA 2006/07 NCHINI TANZANIA?

VYOMBO VYA HABARI MTANDAONI

  • The Citizen
  • Mwananchi
  • Mwanaspoti
  • Business Times
  • Majira
  • Daily News
  • Nipashe
  • The Guardian
  • The Express
  • Kiongozi
  • Uhuru/Mzalendo
  • Arusha Times
  • BLOGI ZA KISWAHILI

  • Bangaiza
  • Mwandani
  • Pambazuko
  • Damija
  • Mtafiti
  • Martha
  • Gaphiz
  • Swahili time
  • Miruko
  • Dira yangu
  • Msangimdogo
  • Jeff Msangi
  • Kasri la mwanazuoni
  • Kurunzi
  • Baragumu
  • Mawazohuru
  • Fikra Thabiti
  • Mtandaoni
  • Motowaka
  • Mkwinda
  • Ngurumo
  • Nyembo
  • Bwaya
  • Omega
  • Tafakari za Maisha
  • Nuru akilini
  • Mtandawazi
  • Mhujumu
  • Vijimamboz
  • Wakati wa Ukombozi
  • Kijiwe Joto
  • Watoto Wetu
  • Jungu kuu
  • Kisima cha Weledi
  • Jarida la Ughaibuni
  • Bhalezee
  • Sauti ya Baragumu
  • Kona yangu
  • Furahia Maisha
  • Bakanja
  • Terrie Swai
  • Fatma Karama
  • Kazonta
  • Binti Afrika
  • Blogu ya Kilimo
  • Ukombozi
  • Mwafrika
  • Digital Africa
  • Blogu ya lugha mseto
  • BLOGI ZA WAAFRIKA

  • BLOGAFRICA
  • BLOGU ZA WAAFRIKA
  • DIGITAL AFRICA
  • MAMA JUNKYARD'S
  • MSHAIRI
  • KENYAN PUNDIT
  • MONGI DREAMS
  • ISARIA MWENDE
  • CUNNING LINGUISTICA
  • ETHIOPUNDIT
  • MOCHALICIOUS
  • UNGANISHA
  • DEMOKRASIA KENYA
  • CHANUKA
  • BANKELE
  • MAARIFA/AKIEY
  • AFROMUSING
  • NEHANDA DREAMS
  • BLACK LOOKS
  • YUMMY WAKAME
  • AFRICAN OIL POLITICS
  • NUBIAN SOUL
  • SANAA
  • VIRTUAL INSANITY
  • MENTAL ACROBATICS
  • KENYA UNLIMITED
  • JIKUMBUSHE KAZI ZANGU ZA ZAMANI

    April 2006 May 2006 June 2006 October 2007 November 2007 December 2007 May 2008 July 2008 October 2008 July 2009 August 2012 October 2012

    Imetengenezwa na

    Ukibofya hapa utapelekwa katika Blogi ya msangimdogo

    na inawezeshwa na